UKOO WA KINYAHA.

– Ukoo wa Kinyaha ni ukoo unaopatikana kwa uchache sana Uchaggani katika maeneo ya katika ya Uchagga. Huu ni ukoo wenye watu wengi makini na wanaofanya vizuri sana kitaaluma wakiwa wanafanya vizuri sana katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kinyaha unafahamika kwamba miaka ya zamani sana takriban miaka 400 iliyopita uliweka makazi yale ya kudumu katika maeneo ya kijiji cha Lyamrakana, Marangu upande wa kusini maeneo ambayo kwa sasa ni kijiji cha Sembeti. Wakati huo koo tatu zilikuwa zinaishi kama ndugu kwa ushirikiano mkubwa eneo la Lyamrakana walikuwa ni Mboro, Tillya na Kinyaha.

– Lakini baada ya muda kupita na ukoo wa Lyimo kwa kutumia mbinu mbalimbali na hila wakafanikiwa kuuangusha ukoo wa Mboro ambao ulikuwa umeimarisha sana mahusiano yao na ukoo wa Tillya na Kinyagha. Baada ya ukoo wa Tillya kuona ukoo wa Lyimo umepata nguvu kubwa hapo Lyamrakana waliamua kuungana nao na kusaliti mahusiano imara yaliyokuwepo kati yao na ukoo wa Kinyagha.

– Kwa shinikizo kutoka kwenye ukoo wa Lyimo, kiongozi wa ukoo wa Kinyagha aliuawa na ukoo wa Tillya na hivyo watu wa ukoo wa Kinyagha walisambaratika kutokea Lyamrakana kuelekea maeneo mengine. Moja ya watu maarufu wa ukoo wa Tillya waliokimbia Lyamrakana Marangu ni Moye ambaye alikimbilia Kilema na kuweka makazi ya kudumu huko. Hata hivyo baadaye Moye alikuja kuwapokea watu wengine wa ukoo wa Lyimo Kilema waliokimbilia huko kutokea Marangu na kuungana nao kupata ushawishi mkubw abila kujali yale yaliyotokea miaka ya nyuma huko Marangu.

– Hivyo ukoo wa Kinyagha japo wengine waliendelea kubakia katika kijiji cha Sembeti na Lyamrakana, Marangu lakini wengine walikimbilia maeneo mengine ili kupata utulivu wa kuweza kuishi.

– Hivyo ukoo wa Kinyaha unapatikana kwa kiasi katika maeneo ya vijiji vya Lyamrakana au Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Kinyaha unapatikana pia kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Kinyaha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kisaseni, Old Moshi.

Ukoo wa Kinyaha ni ukoo uliosambaratika na kupotea sana, tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo huu ili kuhakikisha kuna maudhui ya kutosha yanayopatikana ambayo yanaweza kuongeza hamasa na shauku ya wachagga na watu wengine kwa ujumla kujifunza zaidi. Maudhui haya yanalenga pia kujenga hamasa na ari ya kuzidi kufanya vizuri sana kwenye maisha.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kinyaha.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kinyaha?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kinyagha?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kinyagha?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kinyaha una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kinyaha wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kinyaha kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kinyagha?

9. Wanawake wa ukoo wa Kinyaha huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kinyagha?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kinyagha?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kinyaha?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kinyagha kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *