UKOO WA MWACHA.

– Mwacha ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Mwacha umekuwa ni ukoo wa watu wajasiri sana kama ilivyo kwa koo nyingi za eneo hilo na pia una watu wengi wanaofanya vizuri sana katika shughuli za biashara na ujasiriamali ndani na nje ya Kilimanjaro.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mwacha unasemekana kwamba ulitokea upande wa mashariki na kuweka makazi ya mwanzo na ya kudumu katika eneo ambalo ilikuwepo himaya ya umangi Kindi. Baadhi ya taarifa zinasema kwamba wachagga wa ukoo wa Mwacha walitokea maeneo ya Vunjo lakini wachagga wenyewe wa ukoo wa Mwacha kupitia kwa wazee wa ukoo wanaamini ukoo wa Mwacha walitokea Old Moshi kuhamia maeneo hayo ya Kibosho.

– Hii ni kwa sababu wazee wa ukoo kutokea kwenye vizazi vilivyopita wanasema kwamba ukoo wa Mwacha ni tawi lililotokea kwenye ukoo wa Macha unaopatikana kwa wingi sana upande wa mashariki hususan katika eneo la Mbokomu, Old Moshi na Kirua Vunjo kuelekea mashariki zaidi. Wachagga wa ukoo wa Mwacha sehemu za Kibosho wanaamini kwamba ukoo wa Macha ni ndugu zao wa damu na ndio chimbuko lao halisi walikotokea na kuelekea magharibi.

– Tawi lingine la ukoo ambalo linaaminika limetokea kwenye ukoo wa Mwacha uliotokea kwenye Macha likaelekea tena upande wa magharibi zaidi katika kijiji cha Shari, Machame katika karne ya 17 na baadaye katika karne ya 18 wakaelekea magharibi zaidi na kusambaa katika vijiji vya eneo la Masama ya leo hususan katika vijiji vya Mudio na Saawe ni ukoo wa Mwasha. Inafahamika kwamba tofauti kati ya ukoo wa “Mwacha” na “Mwasha” ni matamshi tu ya lugha ya kichagga cha eneo husika. Yaani ile misamiati ambayo Kibosho mzizi wa neno ni “ch” kwa Machame hutumia “sh”, kwa mfano neno “Weka Vizuri” kwa kichagga Kibosho husema “Wika Nicha” wakati kwa kichagga Machame husema “Wika Nisha” au neno “Mtu Mbaya” Kibosho husema “Mndu Mbicho” wakati Machame husema “Mndu Mbisho” n.k.,. Sasa utofauti huo ndio uliotokea kwenye jina la ukoo kati ya “Mwacha” na “Mwasha” kutokana na maeneo wanakopatikana na matamshi ya lugha ya kichagga inavyoyatamka. Vinginevyo ukoo huu unaaminika kuwa ni kitu kimoja katika Uchaggani, Kilimanjaro yote.

– Ukoo Mwacha ambao miaka ya zamani ulikuwa ni ukoo mashuhuri sana ndani ya iliyokuwa himaya ya umangi Kindi ambayo baaadaye ilikuja kuwa sehemu ya Kibosho ulikuwa unatoa wapiganaji hodari sana ambao waliweza kuimarisha sana himaya hii iliyokuwa imara sana katikati ya himaya mbili kubwa za umangi zenye nguvu sana za Kibosho upande wa mashariki na Machame upande wa magharibi. Ukoo wa Mwacha umeendelea kukua na kusambaa katika maeneo mengi zaidi ya ukanda huu na unapatikana kwa wingi na kwa uchache katika vijiji mbalimbali.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Umbwe, kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kindi Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Msasani, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana katika kijiji cha Omarini, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Dakau, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Uri, Kibosho. Kijiji cha Uri, Kibosho kimetawaliwa na koo mbili kubwa sana Mwacha na Mselle na kwa kiasi Temba.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

– Ukoo wa Mwacha unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mweka, Kibosho.

Pamoja na kuwa na taarifa kiasi kutoka kwa wachagga wa ukoo wa Mwacha wa kizazi hiki juu ya chimbuko na kusambaa kwa ukoo wa Mwacha lakini bado kuna taarifa nyingi zisizojulikana namna ukoo huu ulivyotokea na matawi yake. Tunahitaji kufahamu zaidi taarifa juu ya ukoo wa Mwacha zitakazosaidia kujenga uelewa wa ukoo huu sambamba na kujenga hamasa zaidi, umoja na mshikamano juu ya wanaukoo kuelekea kufanikisha mambo mengi mazuri ya pamoja na ya mtu mmoja mmoja katika ukoo. Taarifa zitakazoongeza mengi kwenye tafiti, kuongeza maudhui na kukuza maktaba ya wachagga, Kilimanjaro kuendelea kujitambua na kurudisha umoja wenye nguvu zaidi.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mwacha.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mwacha?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mwacha?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mwacha?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mwacha una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mwacha wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mwacha kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mwacha?

9. Wanawake wa ukoo wa Mwacha huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mwacha?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mwacha?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mwacha?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mwacha kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *