UKOO WA LEMA.

– Ukoo wa Lema ni ukoo mkubwa sana wa wachagga mashuhuri na wenye heshima kubwa sana ndani na nje ya Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Lema wamekuwa ni watu wapambanaji na wenye msimamo thabiti katika mambo ya msingi tangu karne nyingi zilizopita mpaka sasa. Ukoo wa Lema una watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri katika nyanja …

UKOO WA TEMBA.

– Ukoo wa Temba ni ukoo mkubwa sana maarufu na mashuhuri unaopatikana kwa wingi zaidi katikati na katikati magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa wenye watu wengi sana wanaofanya kazi maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Temba kwa uchaggani unasemekana kwamba ulikuwa …

UKOO WA SHOO.

– Ukoo wa Shoo ni ukoo mkubwa na mashuhuri sana wa kichagga unaopatikana kwa wingi zaidi Machame na kwa kiasi maeneo mengine mbalimbali ya Uchaggani, Kilimanjaro. Ukoo wa Shoo umekuwa ukisifika kama ukoo wenye watu wengi makini wenye kujituma sana na wanaofanya vizuri sana katika maisha. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Shoo unatajwa kuwa …

UKOO WA MLAY.

– Ukoo wa Mlay ni ukoo mkubwa na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki na kati wa Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Mlay unasemekana kwamba ndio ukoo mkongwe zaidi katika …

UKOO WA MUNISI/NKYA/NYARI.

– Baadhi ya watu hawajui kwamba Munisi, Nkya na Nyari ni ukoo mmoja licha ya kuonekana kama koo tofauti kwa watu wasiozijua. Hivyo licha ya zile sababu ambazo watu wanasema kuwa ndio chanzo cha utofauti wa ukoo huu uliogawanyika tutaujadili kama ukoo mmoja na wahusika wanaweza kutueleza sababu ya wao kuwa na majina matatu tofauti …

UKOO WA MTUI.

– Ukoo wa Mtui ni ukoo mkongwe sana na uliokuwa mashuhuri sana zamani Uchaggani. Huu ni ukoo mkubwa na maarufu sana katika vijiji vingi vya upande Kaskazini wa himaya ya umangi Marangu. Wachagga wa ukoo wa Mtui walifahamika kwa uwezo mkubwa kiakili, kiuongozi na hata kivita tangu karne nyigi zilizopita huko Uchaggani, Kilimanjaro. – Makazi …

UKOO WA MAKERE.

– Ukoo wa Makere ni ukoo wa wachagga unaopatikana zaidi katika kijiji cha Sonu na Ngira, Masama au Machame ya magharibi. Ukoo wa Makere unasemekana kuwa ni tawi la ukoo wa Mboro lililoweka makazi yake ya mwanzoni katika kijiji cha Ngira na Sonu. – Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba tawi hili la ukoo wa Makere …

UKOO WA MBUYA.

– Ukoo wa Mbuya ni ukoo mkubwa unaopatikana zaidi katika eneo la katikati ya Kilimanjaro. Yaani ukoo wa Mbuya umesambaa katika eneo kubwa la uchagga la katikati lakini haupatikani sana magharibi ya mbali wala mashariki ya mbali. – Wachagga wa ukoo wa Mbuya wamekuwa ni watu wenye kujituma na wapenda maendeleo na inafahamika kwamba msomi …

UKOO WA MASSAWE.

– Ukoo wa Massawe ni ukoo mkongwe sana na unaweza kuwa ndio ukoo maarufu kuliko zote Uchaggani. Lakini ukoo wa Massawe pia ndio ukoo unaopatikana maeneo mengi na vijiji vingi uchaggani pengine kuliko zote. Kwanza sio rahisi kukuta eneo la uchagga Kilimanjaro lisilo na ukoo wa Massawe kabisa japo kuna maeneo ambayo ukoo wa Massawe …