One of the Greatest Sons of Kilimanjaro. – Wachagga na Sifa Ya Kipekee Sana Kama Jamii Ya Wazawa Ndani Ya Nchi Hii Inayofanya Vizuri Sana Kwenye Sekta Binafsi. Pamoja na Mitazamo Hasi na Chuki za Baadhi Ya Watu Kwa Jamii Hii Bado Kwa Sehemu Kubwa Ndio Viongozi Katika Maeneo Mengi Kwenye Sekta Binafsi Nchini. – …
HADITHI YA ZAMANI YA WACHAGGA “CHAGGA LEGEND” KUHUSU NAMNA MLIMA KILIMANJARO ULIVYOTOKEA.
Siku zote huwa ni kawaida kwa watu wa jamii kuwa na hadithi zao za kale (legends) ambazo huwa ziko kama utani lakini zilizobeba mafundisho fulani ya kwenye jamii. Tunafahamu kwamba kuna hadithi maarufu ya wachagga kuhusu “Kibo na Mawenzi” ambavyo ni vile viwili vya juu vya mlima Kilimanjaro inayoelezea sababu ya vilele vile kuwa na …
UKOO WA KITALI.
– Kitali ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa kiasi katika maeneo ya mashariki ya karibu, mashariki ya kati na mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kitali wamesambaa kwa kiasi katika baadhi ya vijiji lakini vinavyopatikana mbalimbali sana kuelekea upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kitali wanafanya shughuli …
UKOO WA LASWAI.
– Laswai ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa wingi kiasi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro hususan maeneo ya katikati ya ukanda huu wa mashariki ya mbali ya Uchagga. Wachagga wa ukoo wa Laswai ni watu wachangamfu, wajasiriamali wazuri na baadhi wamefanikisha mambo makubwa sana kwenye maisha. – Kutoka kwenye historia ukoo …
UKOO WA MROSSO.
– Mrosso ni ukoo mkubwa, mashuhuri na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa zaidi upande wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliosambaa katika maeneo ya vijiji vingi sana vya mashariki ya Uchagga kwa wingi kwenye baadhi ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingine. – Wachagga wa ukoo wa Mrosso wengi …
BINADAMU ALIYEISHI MIAKA MINGI ZAIDI DUNIANI KATIKA HISTORIA NI MCHAGGA.
– Katika miaka ya 1930’s aliyekuwa kiongozi mkuu wa serikali ya Waingereza Kilimanjaro Sir Charles Dundas alitembelea Uchaggani katika eneo la Mbokomu, Old Moshi lililopo mashariki ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro, ambapo katika ziara yake Dundas alikutana na Mzee mmoja aliyeitwa Mrukumu ambaye alikuwa na umri wa kati ya miaka 110 mpaka 120. – Umri …
UCHUMBA MPAKA NDOA KWA WACHAGGA.
2. NDOA. SEHEMU YA 1. – Baada ya taratibu zote za mambo ya uchumba na ndugu wote wa bibi harusi wanaopaswa kupewa kile wanachostahili kumalizika sasa umefika wakati wa bwana harusi wa kichagga kumdai ili kukabidhiwa bibi harusi wake. Tangazo la ndoa hupelekwa kwa wazazi wa bibi harusi kupitia Mkara(mdhamini) kwenda kwa baba wa binti …
LEO KATIKA HISTORIA – KILIMANJARO, WACHAGGA NA MLIMA KILIMANJARO.
– Siku Kama Ya Leo Ilikuwa ni Tarehe 11/May Ya Mwaka 1848, Ikiwa ni Miaka 185 Iliyopita Kufikia Siku Ya Leo, Mtu Kwanza Kutokea Nchi za Magharibi Mmisionari wa Kijerumani Johannes Rebmann Aliouona Mlima Kilimanjaro(Aliuita Mlima wa Wachagga(Mountain of the Chagga)) na Kwa Mara Ya Kwanza Mlima Kilimanjaro Ukaanza Kufahamika Kwenye Dunia Ya Magharibi na …
UKOO WA MWANGA.
– Mwanga ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa magharibi ya kati kuelekea magharibi ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro kwa wingi katika baadhi ya vijiji na kwa uchache katika vijiji vingine. Baadhi ya wachagga wa ukoo wa Mwanga ni watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili na waliojaliwa vipaji vikubwa katika taaluma …
NGUVU YA MAANDISHI NA SALAMU ZA MEI MOSI.
– Siku moja ilikuwa ni mida ya jioni tulikuwa tunafanya maongezi ya kubadilishana mawazo na rafiki yangu mmoja kuhusu mambo mbalimbali katika maisha. Tuliongea mambo mengi sana kwa kirefu lakini ghafla uelekeo wa mazungumzo ukabadilika tukaanza kujadili kuhusu jamii ya wachagga na mambo yao pamoja na mwenendo wa kule wanakoelekea kwa sasa. – Rafiki yangu …