– Kweka ni ukoo maarufu na mkubwa sana unaopatikana kwa wingi upande wa magharibi ya Uchaggani, Kilimanjaro. Wachagga wengi wa ukoo wa Kweka ni watu wenye nidhamu ya kazi na wenye kujituma wakiwa wamesambaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na katika maeneo yote ya nchi na hata nje ya Tanzania. – Kutoka kwenye …
Category: Makala
RAI YA MWAKA MPYA.
Tujenge Utamaduni wa Kusoma, Tukuze Uwezo wa Kusoma. – Kiasili kila kiumbe ameendeleza uimara katika eneo fulani la mwili wake au maeneo fulani ya mwili wake yanayomwezesha kukabiliana na mazingira anayoishi na hivyo kuishi kwa ubora zaidi. Kwa mfano baadhi ya wanyama wana nguvu, mbio, meno na makucha yanayowawezesha kuwinda wanyama wengine kwa mafanikio na …
BIBI MAKIMARO KALANGA.
– Mimi na rafiki yangu pamoja na rafiki zetu siku ya mwaka mpya 2023 tulifanikiwa kutembelea huko mitaa ya Kibosho katika kijiji cha Kirima kati, Kida Chini na kukutana na bibi mmoja mcheshi, mchangamfu na mwenye akili sana. Bibi huyu mjasiriamali na mpambanaji sana anayeitwa Makimaro Kalanga ana wastani wa umri wa miaka kati ya …
UKOO WA SHIRIMA
– Shirima ni ukoo maarufu na mashuhuri sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Shirima ni kati ya koo za wachagga ambazo kongwe, kubwa, mashuhuri na maarufu sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Ukoo wa Shirima pia ni ukoo wenye watu maarufu na wenye mafanikio makubwa ukiwa …
UKOO WA LYATUU.
– Ukoo wa Lyatuu unafahamika kama kati ya koo kongwe zenye chimbuka lake katika eneo la vijiji vya Tsudunyi na Mahoma, Old Moshi. Wachagga wa ukoo wa Lyatuu wanasemekana kwamba walikuwa ni kati ya koo zilizowezesha katika kuimarika kwa taasisi ya umangi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi. – Kutoka kwenye historia wachagga wa ukoo …
UKOO WA OLOTU.
– Ukoo wa Olotu/Ulotu ni tawi la ukoo wa Mallya lenye chimbuko lake katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho katika eneo lenye umaarufu zaidi kama Kibosho Maro. Zamani wakijulikana zaidi kama ukoo wa Olotu Mallya hawa ni wachagga wenye ujasiri mkubwa sana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha ni kati ya koo za wachagga zenye …
UKOO WA MALLYA.
– Ukoo wa Mallya ni ukoo mkubwa mashuhuri na maarufu sana Uchaggani kwa ujumla. Huu ni ukoo unaohusishwa na watu wengi wenye ujasiri mkubwa katika kukabiliana na mambo mbalimbali katika maisha kwa ujumla. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Mallya kwa Uchaggani, Kilimanjaro unaonekana kuwa na chimbuko lake katika vijiji vya ukanda wa juu Kibosho …
HUU MTAZAMO HASI UNABOMOA ZAIDI KULIKO KUJENGA.
– Ni rahisi kusambaza picha kama hizi ambazo zinaonekana kama ni za kuchekesha japo humjui nani aliyezitengeneza na alikuwa na lengo gani. Kuna uwezekano picha hizi huwa zinatengenezwa na mtu/watu wenye malengo ya kuharibu taswira nzima ya hili suala la kurudi nyumbani ili kudhoofisha au kuionyesha jamii kwamba hayo ndio haswa yanayofanyika. – Je, katika …
*KITABU CHA “MIAKA 700 YA WACHAGGA” – MOSHI.*
– Hiki ndio kipindi katika mwaka ambacho wachagga wanapatikana kwa wingi zaidi Moshi kuliko wakati mwingine wowote. Kwa kutambua hilo tumejitahidi kuhakikisha kwamba nakala kadhaa zinapatikana Moshi japo sio kwa wingi sana kutokana na stock hii ya awamu ya tatu kuelekea kumalizika. – Hivyo kwa wale wenye kutokea mbali na wale wenye kutaka kununua moja …
UKOO WA MSELE.
– Ukoo ni ukoo mkubwa na maarufu sana Kibosho na unasemekana kuwa ndio ukoo mkongwe zaidi Kibosho kwa kupitia kuhesabu vizazi. Inasemekana kwamba mwanzoni ukoo wa Msele walikuwa wanaishi katika ukanda wa juu wa kijiji cha Uri, Kibosho ambapo kwa sasa ni eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro kabla ya kushuka na kuweka makazi ya …