UKOO WA MLAY.

– Ukoo wa Mlay ni ukoo mkubwa na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki na kati wa Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Mlay unasemekana kwamba ndio ukoo mkongwe zaidi katika …

UKOO WA MUNISI/NKYA/NYARI.

– Baadhi ya watu hawajui kwamba Munisi, Nkya na Nyari ni ukoo mmoja licha ya kuonekana kama koo tofauti kwa watu wasiozijua. Hivyo licha ya zile sababu ambazo watu wanasema kuwa ndio chanzo cha utofauti wa ukoo huu uliogawanyika tutaujadili kama ukoo mmoja na wahusika wanaweza kutueleza sababu ya wao kuwa na majina matatu tofauti …

UKOO WA MTUI.

– Ukoo wa Mtui ni ukoo mkongwe sana na uliokuwa mashuhuri sana zamani Uchaggani. Huu ni ukoo mkubwa na maarufu sana katika vijiji vingi vya upande Kaskazini wa himaya ya umangi Marangu. Wachagga wa ukoo wa Mtui walifahamika kwa uwezo mkubwa kiakili, kiuongozi na hata kivita tangu karne nyigi zilizopita huko Uchaggani, Kilimanjaro. – Makazi …

UKOO WA MAKERE.

– Ukoo wa Makere ni ukoo wa wachagga unaopatikana zaidi katika kijiji cha Sonu na Ngira, Masama au Machame ya magharibi. Ukoo wa Makere unasemekana kuwa ni tawi la ukoo wa Mboro lililoweka makazi yake ya mwanzoni katika kijiji cha Ngira na Sonu. – Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba tawi hili la ukoo wa Makere …

UKOO WA MBUYA.

– Ukoo wa Mbuya ni ukoo mkubwa unaopatikana zaidi katika eneo la katikati ya Kilimanjaro. Yaani ukoo wa Mbuya umesambaa katika eneo kubwa la uchagga la katikati lakini haupatikani sana magharibi ya mbali wala mashariki ya mbali. – Wachagga wa ukoo wa Mbuya wamekuwa ni watu wenye kujituma na wapenda maendeleo na inafahamika kwamba msomi …

UKOO WA MASSAWE.

– Ukoo wa Massawe ni ukoo mkongwe sana na unaweza kuwa ndio ukoo maarufu kuliko zote Uchaggani. Lakini ukoo wa Massawe pia ndio ukoo unaopatikana maeneo mengi na vijiji vingi uchaggani pengine kuliko zote. Kwanza sio rahisi kukuta eneo la uchagga Kilimanjaro lisilo na ukoo wa Massawe kabisa japo kuna maeneo ambayo ukoo wa Massawe …

UKOO WA NDOSSA.

– Ukoo wa Ndossa ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo mkubwa kiasi Machame ya magharibi na mashariki ukiwa na ngome yake katika kijiji cha Saawe, Masama. – Watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya ukoo huu wa Ndossa na ukoo wa Ndosi …

UKOO WA SIAO.

– Ukoo wa Siao ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao sio maarufu sana lakini unapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji. – Wachagga wa ukoo wa Siao wanapatikana Masama magharibi katika kijiji cha Lukani na vijiji jirani. Hakuna taarifa nyingi zinazopatikana juu ya makazi ya asili Uchaggani …

UKOO WA MWASHA

– Ukoo wa Mwasha ni ukoo maarufu na mkongwe sana uchaggani hususan katika upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Mwasha ambao wanapatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Mudio, Masama au Machame ya magharibi kwa ujumla ni watu makini na wenye kujituma sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi wanakopatikana. …