UKOO WA MTUI.

– Ukoo wa Mtui ni ukoo mkongwe sana na uliokuwa mashuhuri sana zamani Uchaggani. Huu ni ukoo mkubwa na maarufu sana katika vijiji vingi vya upande Kaskazini wa himaya ya umangi Marangu. Wachagga wa ukoo wa Mtui walifahamika kwa uwezo mkubwa kiakili, kiuongozi na hata kivita tangu karne nyigi zilizopita huko Uchaggani, Kilimanjaro. – Makazi …

UKOO WA MAKERE.

– Ukoo wa Makere ni ukoo wa wachagga unaopatikana zaidi katika kijiji cha Sonu na Ngira, Masama au Machame ya magharibi. Ukoo wa Makere unasemekana kuwa ni tawi la ukoo wa Mboro lililoweka makazi yake ya mwanzoni katika kijiji cha Ngira na Sonu. – Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba tawi hili la ukoo wa Makere …

UKOO WA MBUYA.

– Ukoo wa Mbuya ni ukoo mkubwa unaopatikana zaidi katika eneo la katikati ya Kilimanjaro. Yaani ukoo wa Mbuya umesambaa katika eneo kubwa la uchagga la katikati lakini haupatikani sana magharibi ya mbali wala mashariki ya mbali. – Wachagga wa ukoo wa Mbuya wamekuwa ni watu wenye kujituma na wapenda maendeleo na inafahamika kwamba msomi …

UKOO WA MASSAWE.

– Ukoo wa Massawe ni ukoo mkongwe sana na unaweza kuwa ndio ukoo maarufu kuliko zote Uchaggani. Lakini ukoo wa Massawe pia ndio ukoo unaopatikana maeneo mengi na vijiji vingi uchaggani pengine kuliko zote. Kwanza sio rahisi kukuta eneo la uchagga Kilimanjaro lisilo na ukoo wa Massawe kabisa japo kuna maeneo ambayo ukoo wa Massawe …

UKOO WA NDOSSA.

– Ukoo wa Ndossa ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo mkubwa kiasi Machame ya magharibi na mashariki ukiwa na ngome yake katika kijiji cha Saawe, Masama. – Watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya ukoo huu wa Ndossa na ukoo wa Ndosi …

UKOO WA SIAO.

– Ukoo wa Siao ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao sio maarufu sana lakini unapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji. – Wachagga wa ukoo wa Siao wanapatikana Masama magharibi katika kijiji cha Lukani na vijiji jirani. Hakuna taarifa nyingi zinazopatikana juu ya makazi ya asili Uchaggani …

UKOO WA MWASHA

– Ukoo wa Mwasha ni ukoo maarufu na mkongwe sana uchaggani hususan katika upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Mwasha ambao wanapatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Mudio, Masama au Machame ya magharibi kwa ujumla ni watu makini na wenye kujituma sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi wanakopatikana. …

UKOO WA NDOSI.

– Ukoo wa Ndosi ni ukoo mkongwe sana na unaopatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mbweera, Masama kati. Ukoo wa Ndosi ni tawi la ukoo wa Mboro ambao tulishaujadili hapa kwa kina na matawi yake lakini tawi lilikuwa na nguvu sana katika eneo hili la Masama kati na ndio ulikuwa ukoo wa watawala eneo …

UKOO WA NG’UNDA.

– Ukoo wa Ng’unda ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika vijiji vya Masama Magharibi kama vile Ng’uni. Huu ni ukoo ambao sio mkubwa sana lakini una watu wengi makini unaoweza kukutana nao katika maeneo mbalimbali. – Hakuna taarifa za kutosha sana kujua chanzo chake halisi au kama huenda ni tawi la ukoo mwingine mkubwa zaidi …