HADITHI ZA DINI YA ASILI YA WACHAGGA KABLA YA KUJA KWA WAMISIONARI WA KIKRISTO – 2

Baada ya Ruwa/Iruwa kupotea na kutoonekana tena kiongozi mkuu wa wachagga aliamua kusali kwa kumwomba Ruwa/Iruwa kwa ajili ya asali na maziwa. Ruwa/Iruwa alisikia sala hiyo na kumtuma tena waziri wake msaidizi kwa kiongozi mkuu wa wachagga. Ruwa/Iruwa alimtuma waziri akamwaambie kiongozi mkuu wa wachagga, “Sasa nimeamua kuwaonea huruma wewe na watu wako. Kuanzia sasa …

HADITHI ZA DINI YA ASILI YA WACHAGGA KABLA YA KUJA KWA WAMISIONARI WA KIKRISTO. – 1

Kama tunavyofahamu kila dini duniani ina hadithi zake za mambo ambayo yanaaminika kwamba yalitokea zamani ambazo ndizo zinajenga misingi ya dini husika. Kwa upande wa dini ya kikristo kuna hadithi za mambo yaliyotokea zamani ndani ya jamii ya Wayahudi au Waisrael ambazo zinahusianishwa na Mungu wa wakristo moja kwa moja. Hadithi zilizoanzia kwenye jamii ya …

WIVU WA ASILI.

Wote Tunafahamu Kwamba Binadamu Ni Viumbe wa Hisia. Lakini Katika Moja Ya Hisia Zenye Nguvu Sana Ndani Ya Binadamu Ni Pamoja na Hisia Za Wivu. Hisia za Wivu Ni Zile Hisia Ambazo Huamka Ndani Ya Mtu Pale Anapogundua Kwamba Mtu Mwingine Amemzidi Katika Eneo Fulani. Hizi Ni Hisia Ambazo Binadamu Wote Huwa Tunazo Ndani Yetu.Lakini …

KURUDISHA NA KUDUMISHA UKUU NA UIMARA WA WACHAGGA KUPITIA KOO.

Tunapozungumzia Uimara wa Wachagga Watu Wengi Wana Mtazamo wa Uimara wa Kiuchumi Zaidi au Vitu Vinavyoonekana na Kushikika. Lakini Katika Uhalisia Uimara Wetu Sio Maendeleo Ya Kiuchumi Moja Kwa Moja, Maendeleo Ya Kiuchumi ni Matokeo Ya Uimara Katika Maeneo Mengine Ambayo Hayaonekani Kwa Macho Wala Kushikika. Kitu Kikubwa Sana Katika Kujenga Uimara Utakaoleta Ufahari Kama …

ARI YA WACHAGGA “CHAGGA SPIRIT”

Kuna Ambao Walihitaji Ufafanuzi Juu Ya Post Hii Kabla Ya Makala za Historia, Nimeirudisha Tena Baada Ya Makala Za Historia Ili Waliofuatilia Historia Vizuri Waweze Kuirudia Kulinganisha Sasa Kile Walichojifunza na Mtazamo wa Mwandishi Huyu wa Africa’s Dome of Mystery, Eva Stuart Watt wa Miaka Ya 1920’s/1930’s. CHAGGA SPIRITNyakati Zimekuwa Zikibadilika Uchaggani Tangu Karne Nyingi …

Ahsanteni Urithi Wetu Wachagga

Habari Wafuasi wa Urithi Wetu Wachagga. Nachukua Fursa Hii Kuwashukuru Wote Ambao Tumekuwa Pamoja Hapa Kwa Kipindi cha Miezi Miwili Mkifuatana na Sisi Katika Mfululizo wa Makala za Historia Ya Wachagga kwa Kipindi cha Miaka 700 Kadiri Tulivyojaliwa Kukusanya Taarifa. Napenda Niwashukuru Wote Waliofuatilia Mwanzo Mpaka Mwisho Kwani Nyinyi Ndio Sababu Tumeweza Kuweka Mfululizo Huu …

MIAKA 700 YA WACHAGGA.

Miaka 700 Ya Wachagga Ni Mfululizo wa Baadhi Ya Makala Za Historia Ya Wachagga Kwa Wastani wa Kipindi Cha Miaka 700 Kwa Kadiri Tulivyojaliwa Kukusanya Taarifa Kutoka Kwenye Vyanzo Mbalimbali. Ni Kazi Iliyochukua Muda Mrefu na Kuhusisha Kusoma Vitabu Vingi, Kudadisi, Kutafiti, Kutafakari na Kujadili Matukio Mbalimbali Ya Kihistoria Kuhusu Kilimanjaro na Wachagga. Watu Mbalimbali …